Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Nyumba za kuchua misuli Dar zimegeuzwa madanguro

24831 Pic+makonda+3 TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema baadhi ya nyumba za kuchua misuli ‘masaji’ jijini hapa  zimegeuzwa kuwa madanguro na zinatumika kufanyia mambo ya hovyo.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 31, 2018 wakati akitangaza kamati maalumu ya watu 15 iliyoundwa kwa ajili ya kupambana na mapenzi ya jinsia moja, wanaotumia mitandao ya kijamii kujiuza sambamba na wanaotapeli kwa kutumia majina ya watu mashuhuri nchini.

Amesema kwa sasa kuna ongezeko la nyumba hizo katika sehemu mbalimbali jijini humo wakitumia nyumba hizo tofauti na kusudio la kuanzishwa kwake.

“Lazima tujihakikishie kuwa wamesajiliwa, kama wana wataalamu wa massage (kuchua misuli) na wanazingatia taratibu za biashara zao kuliko kuwaacha wafanye mambo yaliyo kinyume na biashara zao,” amesema Makonda.

Amesema kati ya ujumbe mfupi 18,972 zilizotumwa kupitia simu yake ya mkononi zipo nyumba 24 zilizotajwa kuhusika kurekodi picha za ngono.

Chanzo: mwananchi.co.tz