Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Mfumo wa kusukuma maji Mto Msimbazi kujengwa

57417 Pic+makonda

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema Serikali imeanza maandalizi kwa ajili kujenga upya mfumo wa kusukuma maji katika bonde la Mto Msimbazi, sanjari na kuondoa kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo eneo la Jangwani.

Serikali itatekeleza mradi huo baada ya kupata mkopo wa dola 100 milioni kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kumaliza tatizo sugu la mafuriko Jangwani kupitia Mto Msimbazi.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 14, 2019 wakati wa ziara ya ukaguzi wa athari za mvua katika eneo la Jangwani.

Katika ziara hiyo Makonda ameongozana na viongozi mbalimbali wakiwamo wawakilishi wa CCM, idara ya uhamiaji, magereza, askari polisi na watendaji wa taasisi mbalimbali ikiwamo Wakala wa Barabara (Tanroads) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura).

"Kwa sasa wako katika upembuzi yakinifu, tunategemea ndani ya mwezi mmoja wamalize ili waje na ‘design’ inayoweza ku- accommodate mazingira yote ikiwamo Mto Msimbazi.”

"Mto Msimbazi una takribani kilomita 16, mvua inayonyesha katikati ya Dar ni kidogo lakini maji mengi yanatoka Kisarawe na Milima ya Pugu kwa hiyo mradi utaangalia mfumo mzima ili kudhibiti athari za mafuriko,” amesema Makonda.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz