Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Kongamano la uwekezaji sekta ya utalii ni maelekezo ya Rais

Rais Samia: Makonda Umekichemsha Chama Makonda: Kongamano la uwekezaji sekta ya utalii ni maelekezo ya Rais

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Tukio la leo limeasisiwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni muendelezo wa dhamira yake ya kumtengenezea kipato kila mwananchi katika kila daraja (kuanzia mwendesha Bodaboda, mkulima wa mchicha, mwenye kibanda cha Biashara mpaka mwenye Hoteli) na dhamira hiyo imeelezwa na watangulizi wengi waliokuja hapa kuongea ikichochewa na uzalendo wake na mapenzi yake na kwa kuwa yeye ni mama nadhani hamasa iliongezeka zaidi ndani ya moyo wake kutaka Watanzania na wananchi wake waishi katika mazingira mazuri wakijipatia kipato halali bila usumbufu wa aina yoyote" -Makonda

"Nakumbuka nilipoteuliwa moja ya mambo mahsusi aliyoyasema hadharani kwenye ukumbi (kwa sababu yako ya ndani na yako ya nje) aliweka mkazo na akatoa maelekezo kwamba nenda ukashirikiane na Wizara ya Mipango na Uwekezaji ili Arusha ibadilike, na kwa kweli nina kila sababu ya kumshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwanza kwa kuniteua, la pili kwa kunileta kwenye mkoa huu wa kimkakati lakini jambo la tatu kwa support anayotupatia wasaidizi wake kutimiza ndoto aliyonayo" -Makonda

Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Arusha amezungumza hayo leo, Jumanne Aprili 30.2024 alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la uwekezaji wa sekta ya utalii lililofanyika kwenye Hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha

Chanzo: www.tanzaniaweb.live