Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makazi ya watu yazingirwa na tope chafu la mgodini

BWAWA 2 Baadhi ya wakazi wa eneo ambalo limezingirwa na maji machafu ya mgodini

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bwawa la maji machafu katika mgodi wa Williamson Diamond wa mkoani Shinyanga, limepasuka na tope kutiririka kwenye makazi ya watu na kusababisha nyumba 13 kuzingirwa na tope na maji machafu huku wakazi wakilazimika kuyahama makazi yao kwa muda kwa ajili ya usalama.

Ni wakazi wa vijiji vya Mwangolo na Nyenze, Kata ya Mwaduiluhumbo ambao wameiomba serikali kuwapa msaada wa haraka kutokana na nyumba zao kuzungukwa na tope lililotokana na bwawa la kuhifadhi maji machafu katika mgodi wa Williamson kupasuka na kutiririka kwenda kwenye makazi ya watu na kwenye mashamba

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amesema katika uchunguzi wa awali wamebaini nyumba 13 zimezungukwa na maji machafu pamoja na tope na tayari ameunda tume ili kujua kama kuna athari zaidi na chanzo cha bwawa hilo kupasuka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live