Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makarani wanaotembea na vishkwambi maeneo ya starehe waonywa

Babu Pic Data Makarani wanaotembea na vishkwambi maeneo ya starehe waonywa

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka makarani wa sensa mkoani humo kuwa kutokwenda na vishikwambi kwenye maeneo ya starehe ili visiibwe na badala yake wavirudishe nyumbani baada ya kumaliza kazi zao.

Amesema serikali imetumia fedha nyingi kugharamia vifaa hivyo na kuwataka kuwa navyo makini.

Babu ametoa agizo hilo leo Agosti 24, 2022 akiwa wilayani Hai wakati akikagua mwenendo wa shuguli ya sensa inayoendelea hapa nchini.

"Makarani wa sensa mwe makini kwa sababu hivi vishikwambi ni gharama kubwa ambayo serikali imetumia, hivyo sio kwenda navyo sehemu za starehe.

“Hakikisheni mkimaliza navyo kazi mnakwenda kuvihifadhi nyumbani ndio wendelee na mambo yenu mengine," amesema.

Amesema mkoa huo unao ulinzi wa kutosha katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha makarani wanafanya kazi zao katika sehemu salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live