Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamu, Rais, atoa, maagizo, matano, Pwani

24582 Pic+samiaaa TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amempa maelekezo matano Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.

Maelekezo hayo ni pamoja na kujenga au kuboresha vyuo vya ufundi mkoani humo, kusimamia mazingira, kusimamia haki za wafanyakazi, uadilifu kwa wafanyakazi na kujenga mahusiano kati ya sekta binafsi na ya umma.  

Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya viwanda mkoani Pwani.

Amemwambia mkuu huyo wa mkoa awatumie wawekezaji waliopo na wanaokuja kuboresha vyuo vya ufundi vilivyopo ili kuwa na vijana wenye ujuzi.

“Ni kweli tumeona kuna ajira ya Watanzania wengi, baadhi ya viwanda tumekuta wanajitayarisha kutoka na kuachia kwa Watanzania na wao watakuwa waangalizi tu, hili haliji kwa utashi, viwanda hivi haviwezi kumchukua kila mtu bila ujuzi wala taaluma maalumu, nitoe wito kwa mkuu wa mkoa, mna fursa ya kuwatumia wawekezaji ambao wamewekeza na watakaokuja wawasaidie kukiboresha chuo cha ufundi cha mkoa kufundishe waliotoka kidato cha nne na chini ya hapo wawe mafundi wa kuajiriwa kwenye viwanda hivi, ”ameagiza.

Amesema ameona maeneo mengi ya viwanda yanaendelea kupimwa, hivyo hawana budi kutayarisha watumishi watenda kazi watakaoajiriwa kwenye viwanda hivyo, vinginevyo watakuwa watazamaji na watu kutoka mikoa mingine watakuja kuchukua kazi zao.

Suluhu pia alimuagiza mkuu wa mkoa wa Pwani kuhakikisha wafanyakazi wa viwandani wanapata haki zao.

“Wengine wapo kwenye hali nzuri wengine hawapo katika hali nzuri, ningeomba wilaya na taasisi zinazoshughulika na maslahi ya wafanyakazi wazunguke na kuona vijana wanavyohudumiwa, ”amesema.

Amefafanua kuwa wapo wanaoingia zamu saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni, hapa kuna haki zao lazima zipatikane saa za kazi kwa sheria ya Tanzania zimetajwa, kama hivyo kiwanda  kinazalisha kwa zamu hizo lazima haki ipatikane.

Makamu wa Rais pia aliagiza jambo lingine ni kwa wafanyakazi wa viwandani kuhubiriwa uadilifu na uongofu katika kufanya kazi.

Ameagiza pia  mkoa uingie makubaliano na wawekezaji wa viwanda  kuziba mashimo ya madini mbalimbali wanayochimba kwa ajili ya utengenezaji bidhaa zao.

Amefafanua kuwa wawekezaji waendelee kufanya tathmini ya mkakati wa mazingira, licha ya kuwa walifanya vilipojengwa ambapo walipata unafuu na ruhusa ya kujenga viwanda.

“Ingieni makubaliano na wawekezaji wafanye jambo yale mashimo, yapigwe greda kuwe hakuna mashimo au yapandwe miti ili parudi kama palivyokuwa naomba mambo ya mazingira yatiliwe maanani, ”amesema.

Amesisitiza kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri na sekta binafsi na ya umma ili kuongeza ufanisi katika sekta ya viwanda.

“Kupigana vita wenyewe kwa wenyewe wawekezaji hasa wenye viwanda na bidhaa zinazofanana, akiona ubora upo hafifu anatumia nafasi hiyo kumpinga mwenzake, kila mmoja anazalisha kulingana na haki na makubaliano ya nchi, hakuna haja ya kupigana vijembe, ”ameasa Suluhu.

Chanzo: mwananchi.co.tz