Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamba avunja idara ya habari Tanesco

Makambapic Data Waziri wa nishati, January Makamba

Tue, 25 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Waziri wa nishati, January Makamba ameagiza kuvunjwa kwa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kushindwa kulisemea shirika hilo

Makamba ametoa agizo hilo leo Jumanne Januari 25, 2022 wakati alipotembelea kituo cha usambazaji umeme kilichopo Njiro jijini Arusha ambapo amesema amevunja idara hiyo kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yao ikiwemo kulisemea shirika hilo pamoja na kutoa taarifa kwa wateja wao.

"Sisi kama Serikali hatufurahishwi na malalamiko ya wananchi kuhusu kukatika kwa umeme pamoja na upungufu wa taarifa zitolewazo kwa wateja,"amesema Makamba.

Makamba amesema haiwezekani kumgeuza Waziri wa Nishati kuwa msemaji wa Shirika hilo kila inapotokea changamoto.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz