Mkuu wa mkoa wa Mwanza Amos Makalla amemkabidhi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda kitabu chenye malalamiko ya Ardhi yaliyoshughulikiwa na mkoa wake.
Makabidhiano ya kitabu hicho yamefanyika leo tarehe 11 Machi 2024 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Mhe, Pinda kuzindua Klinik ya Ardhi katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Pinda alipongeza mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa juhudi zake za kushughulikia migogoro ya ardhi na kuweka kumbukumbu za kero alizoshughulikia.
‘’Mikoa mingine ingeiga mfano wa mkoa wa Mwanza tungekuwa hatuna kazi kubwa kwa kuwa kutakuwa na kumbukumbu na katika mikoa. Kumbukumbu zitasaidia kupitia wale waliowasilisha migogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makala amesema, ni vizuri wizara ya ardhi pale inapokuta mkoa umefanya maamuzi kuhusiana na migogoro ya ardhi na wizara kupelekewa tena malalamiko basi ni vizuri ikarudi mkoa husika kuulizia ama kufanya mawasiliano kwa nia ya kutafuta njia nzuri ya kushughulikia mgogoro.
‘’Mkiwa wizara mmekuta mkoa ushafanya maamuzi katika masuala ya ardhi halafu watu kwa interest zao wanabeba mgogoro kwa masahi yao ni lazima mrudi kwa mkoa kuuliza mazingira aliyo amua kutoa uamuzi huo’’ alisema Makalla.