Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makalla akerwa wizi miundombinu ya maji

MAKALLA 5?fit=700%2C466&ssl=1 Amos Makalla, RC DSM

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makala amekemea vikali wizi wa miundombinu ya maji ikiwemo mabomba na mita za maji unaoendelea na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kudhibiti wizi huo unaofanywa na watu wasio waaminifu.

Makalla ametoa wito huo leo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji Pugu - Gongo la Mboto hususani kwa wananchi waliounganishwa kupitia mradi huo uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Amesema kuwa wizi wa mabomba na mita za maji umekidhiri na kusababisha usumbufu kwa wateja pamoja na kuleta hasara kwa serikali, ni jambo linalorudisha nyuma nia njema ya serikali kwa wananchi wake.

"Serikali inatumia fedha nyingi kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi na hii ndio kazi inayofanywa na DAWASA, hivyo si vyema kwa mwananchi kuacha mara moja kuhujumu miundombinu ya maji, hili ni ni kosa kisheria," amesema Makalla.

Makala ameipongeza DAWASA kwa kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia fedha za ndani pamoja na ubunifu wa kuwaunganishia wananchi maji kwa mkopo.

Aidha amepongeza uamuzi wa kuhakikisha maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam yanapata huduma ya majisafi.

"Miradi yote ya maji inayotekelezwa pembezoni mwa mji ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma ya majisafi inawafikia wananchi wote, ambapo amewapongeza DAWASA kwa kazi nzuri wanayoifanya.

"Nimepita mtaani kwenye nyumba za wateja na nimeona maji yakitoka tena kwa msukumo mkubwa, niwapongeze sana DAWASA kwa kazi nzuri mnayoifanya," ameeleza.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa Pugu Gongo la Mboto umetekelezwa kwa kutumia shilingi bilioni 7.3 ambazo ni fedha za ndani za Mamlaka.

Mradi umejenga tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni Mwanahamisi Kibuba mkazi wa Kata ya Pugu - mpakani ameishukuru DAWASA kwa kuleta maji kwenye makazi yake na kumuondolea kero ya kutumia maji ya kisima ambayo hayakua masafi.

Ameongeza kuwa maji ya kisima hua sio masafi na hayafai kwa kunywa, pia wakati mwingine hua yanakauka, nimefurahi sana kupata majisafi kutoka DAWASA.

Diwani Kata ya Pugu Imelda samjale amesema mradi wa maji Pugu Gongo la Mboto umekua ni suluhu kwa wananchi wa maeneo haya walioteseka kwa muda mrefu kwa kukosa majisafi.

Ameongeza kuwa DAWASA imetekelezwa kwa mfano mradi huu kwa kutumia fedha za ndani, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kua na matumizi bora ya majisafi.

"Niwaombe DAWASA kuongeza kasi ya kusogeza huduma ya majisafi ili wananchi wengi waweze kuunganishwa kwa kua maji ni yanahitajika sana," amesema.

Nae mkazi wa Pugu Kajiungeni Rachel Clement amesema alikua anatumia fedha nyingi kwa siku kununua maji ya madumu na kumsababishia usumbufu mwingi.

"Nashukuru kwa sasa nimepata majisafi kutoka DAWASA na hivyo imesaidia kupunguza matumizi ya fedha," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live