Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makalla akabidhi Ofisi kwa Chalamila

Chalamila X Makalla Makalla akabidhi Ofisi kwa Chalamila

Thu, 18 May 2023 Chanzo: Dar24

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo Dar es salaam.

Akiongea wakati wa kukabidhi ofisi, Makalla amenukuliwa akisema “Nimesimama hapa kama ushahidi na ishara nzuri ya hii ofisi rasmi kukukabidhi RC Chalamila, najua umeanza kazi na tuliongea kutokana na udharura wake kwamba endelea, nikasema tuje tukabidhiane rasmi, karibu sana Dar es salaam na jisikie nyumbani, wewe ni Mwenyeji sio Mgeni, umesoma hapa kabla ya hapa maisha yako yalikuwa Dar es salaam kwahiyo karibu tena”

“Leo nilikuwa namchekesha namuuliza vihistoria vyetu vinaendana kwanza alikuja nikamkabidhi Mbeya, leo tena namkabidhi Dar es salaam ni Mkoa wa pili namkabidhi”

“Lakini pia tunafanana kitu kingine kwamba tuliwahi kukaa benchi wakati fulani, nilimuuliza ulikaa muda gani akasema mwaka mmoja nikamwambia Mimi miwili, kwahiyo tuna vitabia vya kushabihiana, nakutakia kila la kheri karibu sana Dar es salaam”

Chanzo: Dar24