Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makalla aagiza wakazi dar kuvaa barakoa

2771d1197def8142a816bedfa5d5d258.PNG Makalla aagiza wakazi dar kuvaa barakoa

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameagiza wakazi wa Dar es Salaam kuvaa barakoa kila wakati katika maeneo ya mikusanyiko.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Makalla amewataka Wakuu wote wa Wilaya, Taasisi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kusimamia maelekezo hayo kikamilifu.

Agizo hilo linakuja siku chache baada ya Wizara ya Afya kutoa taarifa za uwepo wa viashiria vya ugonjwa wa corona awamu ya tatu nchini.

Kwa mujibu wa agizo la Mkuu wa Mkoa maeneo yote ikiwemo masoko, mikutano, sherehe, vituo vya kutolea huduma za afya, maofisini, baa, shuleni, vyuoni, migahawa na maeneo mengine.

Chanzo: www.habarileo.co.tz