Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makaburi 777 kuhamishwa kupisha njia ya umeme

Accae937d12c042e30255f343713d456 Makaburi 777 kuhamishwa kupisha njia ya umeme

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPUNI ya Kusambaza Umeme Uganda (UETCL), inafanya mazungumzo na viongozi wa mila na utamaduni katika wilaya ya Acholi na mkoa wa Nile Magharibi, ili kuhamisha makaburi 777 yaliyopo kwenye eneo ambalo njia ya kusafirisha umeme zinajengwa.

Julai 23, mwaka huu, serikali na wadau wa maendeleo walisaini mkataba wa ujenzi wa njia za umeme katika maeneo hayo, kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa umeme kwenye maeneo ya West Nile na Northern Uganda.

Njia ya kusafirisha umeme ya kilovoti 132 itakaojengwa katika eneo la kilometa 294 kutoka Kole-Lira-Gulu hadi Arua, itasafirisha nishati hiyo kutoka mabwawa ya Nyagak na Karuma kwenda mikoa ya West Nile.

Wiki iliyopita, Wizara ya Nishati na maofisa wa UETCL walitembelea maeneo ya mradi huo kumtambulisha mhandisi kwa viongozi wa wilaya wakati serikali ikitarajia kumkabidhi eneo hilo wiki ijayo.

Msemaji wa UETCL, Pamela Byoruganda, alisema makaburi mengi yapo Gulu ambayo ni ya watu waliokufa kwa ebola na uasi wa aina mbalimbali.

Kiongozi wa baraza la jamii ya Koro, huko Gulu, Augustine Ojara, alisema pamoja na fidia ya ardhi, pia wanajadiliana jinsi ya kuhamisha miili ya wapendwa wao.

UETCL ilieleza kuwa, asilimia 75 ya watu 3,333 walioathirika na mradi huo wamelipwa fidia, huku asilimia 25 ya wamiliki hawajabainika na malipo hayo ni mkopo kutoka Benki ya Dunia wa dola za Marekani milioni 100.

Chanzo: habarileo.co.tz