Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maji ya visima kupimwa

Kisima Cha Majiii Maji ya visima kupimwa

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ameziagiza mamlaka za afya na maji wilayani humo kushirikiana na kuainisha idadi ya visima vilivyopo ndani ya wilaya hiyo na kuvipima kubaini maji yake yana usalama kiasi gani kwa matumizi ya binadamu.

DC Jamila ametoa maagizo hayo katika kikao kazi maalum cha kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu, kilichofanyika leo ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mpanda.

Amesisitiza kila kaya kuhakikisha inazingatia suala la usafi wa mazingira, ikiwemo kunawa maji tiririka na kuwataka watumishi kuanzia ya vijiji kuweka nguvu katika suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live