Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maji ya Dk Kijaji kunusuru ndoa

Tue, 9 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kondoa. Wizi wa mifumo ya umeme jua (solar) imetejwa kuwa moja ya changamoto inayoikabili halmashauri ya wilaya ya Kondoa na kusababisha upungufu wa maji maeneo mengi.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na mhandisi wa maji wa halmashauri hiyo, Paraula Seleman alipozungumza na gazeti hili kuhusu miradi ya maji inaoendelea kusuasua.

Seleman alisema Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha maji yanapatikana karibu na wananchi, lakini wanakwama wananchi wanashindwa kulinda mitambo ya umeme jua iliyofungwa kwa ajili ya kusukuma maji.

Alisema kama wizi huo ungedhibitiwa, hakuna shaka maeneo mengi ya Kondoa yangetiririsha maji. “Serikali inasimamia ipasavyo kama ulivyo mbunge (Dk Ashatu Kijaji) umeunga mkono juhudi hizo, lakini hawalindi mitambo hiyo,” alisema Seleman.

Akiwa katika kijiji cha Gayu, Dk Kijaji alikabidhi mradi wa maji na kumaliza tatizo hilo lililokuwa la historia huku akieleza kuwa malalamiko ya wananchi hao yalimnyima usingizi.

Dk Kijaji ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alielezea historia ya eneo hilo kuwa waliishi maisha ya uzamani na ukale kwa kutafuta maji kutwa nzima na kwamba, atahakikisha kila mtaa unafikiwa na miundombinu.

Pia Soma

Naye mkazi wa kijiji hicho, Mariam Idd alisema kupatikana kwa maji hayo ni ukombozi hata kwa ndoa zao kwani kila wakati ilikuwa kelele kutokana na wengi kushinda wakitafuta maji.

Chanzo: mwananchi.co.tz