Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maji bwawa la Mindu yaanza kukauka

Mindu (600 X 450) Maji bwawa la Mindu yaanza kukauka

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Reuben Shigela ametoa maagizo kwa Halmashauri mjini hapo kuwaamisha wananchi wote wanaofanya shughuli katika mito yote inayotiririsha maji kuelekea kwenye bwawa la Mindu.

Amtoa agizo hilo kufuatia kupungua kwa kina cha maji katika bwawa hilo kufuatia mabadiliko ya tabianchi pamoja na hughuli za kibinadamu ambazo sio rafiki kwa vyanzo vya maji.

Shingela kwa kushirikiana na mamlaka za uhifadhi wa bonde la Wamiruvu na Moruwasa wameazimia kuhakikisha wananchi hao wanaondoka katika mameneo hayo mara baada ya kujionea upungufu mkubwa wa maji katika bwawa hilo.

"Kwanza tuzuie shughuli zote za kibinadamu zinazofanywa katika bwawa hili, uwe unalima uwe unachimba madini inabidi usitishe, lengo la bwawa hili ni kuhudumiwa wananchi kwanza, watu hawawezi kukosa maji ya kunywa alafu tunaangalia" Amesema RC huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live