Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeruhi saba ajali ya Mtwara wapewa rufaa, wengine waendelea vizuri

Majeruhi Pic Majeruhi saba ajali ya Mtwara wapewa rufaa, wengine waendelea vizuri

Wed, 27 Jul 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Wanafunzi saba kati ya 17 waliojeruhiwa katika ajaili ya basi la Shule ya Msingi ya King David iliyoua watu 13 wakiwamo wanafunzi 11, wamepewa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhumbili jijini Dar es Salaam na Hospitali ya Rufaa Ndanda, wilayani Masasi kwa matibabu zaidi.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumanne eneo la Mjimwema, Kata ya Mikindani, Mtwara Mjini na kusababisha vifo vya watu 13, kati yao ni wanafunzi 11 wa Shule ya Msingi ya King David na watu wazima wawili, akiwemo dereva wa gari hilo aina ya Toyota Hince na mwanamke mmoja aliyekuwa amepewa lifti

Akizungumza leo Jumatano Julai 27, 2022, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Dk Clemence Haule amesema majeruhi wengine 10 waliobaki katika hospitali hiyo wanaendelea vizuei.

Dk Haule amesema majeruhi mmoja alipewa rufaa jana baada ya kugundulika alipata shida ya shingo na kuvunjika miguu.

“Magonjwa aliyeondoka jana alipata shida ya shingo na kuvunjika miguu ambapo leo asubuhi wawili wameenda pia Muhumbili na wawili wanaenda leo Ndanda kwa matibabu zaidi,” amesema Dk Haule

Chanzo: Mwanaspoti