Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeruhi mmoja ajali ya moto Morogoro afariki, vifo vyafikia 102

72955 Pic+majeruh

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Vifo vinavyotokana na ajali ya lori la mafuta ya petroli iliyotokea Agosti 10, 2019 eneo la Msamvu mkoani Morogoro nchini Tanzania imefikia 102 baada ya majeruhi mmoja kati ya 14 aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kufariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Agosti 26,2019 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha amemtaja aliyefariki ni Grayson Ndabiti (19) hivyo idadi ya majeruhi waliobaki hospitalini hapo ni 13.

Amesema kati ya majeruhi hao saba wako chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine sita wakiwa katika wodi ya Sewahaji.

Chanzo: mwananchi.co.tz