Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeruhi ajali iliyotokea hifadhi ya Serengeti kuhamishiwa Bugando

72382 Ajaliiiipic

Wed, 21 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Baadhi ya majeruhi wa ajali iliyotokea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania wanahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 21, 2019 mganga mkuu wa Hospitali teule ya Nyerere, Tanu Warioba amesema kati ya majeruhi 18, baadhi yao watapelekwa Bugando kwa ajili ya vipimo zaidi.

"Nitatoa taarifa muda si mrefu wangapi wanaenda na kwa nini wanakwenda na wangapi wanabaki," amesema.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumanne Agosti 20, 2019 eneo la Ramai katika hifadhi hiyo wakati wanatoka kuzima moto unaodaiwa kuwashwa na watu wanaodhaniwa  ni majangili.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz