Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeruhi 17 ajali ya basi watoka hospitali

Ajali Majeruhiiiiiiiiii.png Majeruhi 17 ajali ya basi watoka hospitali

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majeruhi 17 kati ya 26 waliofikishwa katika hospitalini ya Nyangao jana, baada ya kupata ajali ya basi la kampuni ya Baraka Classic wameruhiusiwa kutoka baada ya afya zao kuimarika.

Akizungumza na Mwananchi leo, Novemba 27, 2023, Patroni wa Hospitali ya Nyangao, Yosio Mwakyoma amesema majeruhi waliobaki yumo mtoto chini ya miezi mitano ambaye naye anaendelea vizuri.

"Tumebakiwa na majeruhi tisa ambao kati yao wanawake ni watano, wanaume watatu na mtoto mmoja wa kiume. Mgonjwa mmoja mwanaume amefanyiwa upasuaji wa tumbo, yupo chumba cha uangalizi maalumu (ICU), lakini anaendelea vizuri na ameanza kuongea.

“Pia yupo mwanamke mmoja amefanyiwa upasuaji wa mkono naye anaendelea vizuri na wagonjwa wengine hali zao zinaendelea kuimarika," amesema Mwakyoma.

Mwakyoma amesema pia upo mwili wa mzee anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50-60, anayedaiwa alikuwa mpitanjia bado haujatambuliwa.

Majeruhi wasimulia

Arafa Mashughuli, amesema dereva alipoanza kuona breki inafeli, alimwambia kondakta wake aweke jiwe, lakini ilishindikana na kusababisha gari hilo kupata ajali.

"Ajali hii ilianzia mbali, baada ya dereva kuona breki inafeli akamwambia kondakta wake aweke jiwe, lakini ilishindika na kusababisha gari kuteremka hadi kugonga mti ambao ulikuwa na nyuki na kusababisha watu kushindwa kutuokoa kwa haraka," amesema Arafa.

Majeruhi mwingine, Zambda Rashindi amesema gari ilikuwa kwenye mwendo mkali uliosababisha dereva na kondakta kushindwa kushindwa kutoa msaada wowote kutokana na kufeli breki za gari hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live