Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majenereta Kigoma Kuzimwa leo

Mgao Umeme.jpeg Majenereta Kigoma Kuzimwa leo

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hasaan amesema kesho akiwa wilaya ya Kasulu anatarajia kuzima umeme wa jenereta kuashiria mwisho wa matumizi ya umeme huyo na mkoa huo kuanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa.

Rais Samia amesema hayo janaJumapili Oktoba 16, 2022 wakati akizungumza na wananchi katika uwanja cha mpira mjini Kibondo ambapo amebainisha kuwa baada ya kuzindua kituo cha umeme cha Nyakanazi ambacho njia moja wapo ya kufikisha umeme katika mkoa huo, hivyo mkoa wa Kigoma kuwa na njia sita ya kupokea umeme.

Rais Samia amesema mkoa wa Kigoma utakuwa na umeme mwingi na wamefanya hivyo kwasababu wanajua ni mkoa uliopakana na nchi jirani hivyo baadaye na wao watajitaji kununua umeme kutoka nchini Tanzania.

“Tunaleta umeme mwingi Kigoma kwanza kwasababu mkoa umepakana na nchi jirani siku zijazo watakuja kununua umeme kwetu lakini pia uwekezaji uje Kigoma sasa, maji tunashighulika nayo na mambo mengine tunafanyia kazi“amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amesema kwasasa wanataka kuifungua Kigoma kibiashara kutokana na kuwa katika sehemu nzuri na kupakana na nchi jirani ili biashara iweze kushamiri mkoa huo.

Wananchi wa mkoa wa Kigoma wamepata umeme wa gridi ya Taifa kwa mara ya kwanza ambapo awali walikuwa wakitumia umeme wa majenereta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live