Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majanga Mindu kama Hanang?

Minduuuuas Majanga Mindu

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miezi michache baada ya Taifa kushuhudia maafa yaliyotokana na maporomoko ya matope, maji, magogo na mawe yaliyoathiri na kuchukua Maisha ya watanzania kadhaa wakazi Katesh wilayani Hanang mkoani Manyara, hali kama au zaidi ya hiyo inaweza kutokea kwa mamia ya wakazi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi ya Mlima Mindu uliopo Morogoro.

Ni baada ya uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanywa katika eneo hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi wa Morogoro kiasi cha kusababisha makorongo makubwa yanayopitisha maji kutoka mlima Mindu kupeleka mto mindu na baadae bwawa la Mindum aji ambayo huchakatwa pia kwa matumizi ya binaadamu mkoani humo.

Kwa namna gazeti hili lilivyoshuhudia katika ziara maalum ya kujielimisha iliyoandaliwa na taasisi ya Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na taarifa (MECIRA) kwenye mradi wao wa PAZA SAUTI.

Jitihada za dharura zinahitajika kuunusuru mlima huo ambao unazii kuathiriwa kwa kuvamiwa na wananchi wanaoanzisha makazi siku hadi siku huku shughuli za kibinaadam ikiwemo ukataji miti na uchimbaji michanga zikitishia sio tu usalama wa hifadhi ya mlima huo bali hata Maisha ya wakazi wenyewe wa vijiji vinavyouzunguka mlima mindu.

Taarifa zinasema kuwa eneo hilo awali lilikuwa si la makazi ya binadamu, bali kwa sasa binadamu wamevamia, hivyo shughuli za ujenzi, uvunaji wa mchanga, ukataji wa miti na ufugaji kando ya mlima huo, zimeendelea kulifanya kuwa hatarishi Zaidi.

Pamoja na wananchi kujenga kandoni mwa makorongo makubwa yam aji, hali yam to mindu unaotegemewa kupeleka maji bwawa la mindu pia iko hatarini baada ya wakazi kujenga nyumba na kuendeleza mashamba ya mazao mbalimbali mita chache pembezoni mwa mto huo bila kuzingatia sheria zinazowataka wananchi kufanya shughuli za kibinadamu umbali wa mita 60 kutoka katika chanzo cha maji ikiwemo mito, milima, ardhioevu na misitu

Elizaberth Magambo ni mama ambaye amejenga nyumba yake mita tatu tu kutoka usawa wa korongo kubwa linalopitisha maji kutoka mlima mindu ambalo linazidi kuongezeka ukubwa kila mvua zinaponyesha anasema yupo katika hatari na anaiomba Serikali iweze kuwapatia ardhi katika maeneo mengine

“Tupo katika wakati mgumu, tulijua kuwa hii ni kanani yetu lakini imekuwa tofauti, tunatamani kuhama hata kesho ila hatuna uwezo, usiku hatulali hasa kipindi hiki cha mvua, tunaiomba Serikali iingilie kati na kutunusuru kabla mambo hayajaharibika” alisema

Alisema walipohamia eneo hilo halikuwa na makorongo makubwa bali shughuli za binadamu kama vile kuchimba mchanga kwa ajili ya kuuza, ndiyo chanzo kikubwa cha kuharibika kwa eneo hilo.

Uchunguzi wa Mecira umebainisha kuwa pamoja na wakazi wa eneo hilo kuwa karibu kabisa na mlima Mindu hicho kwao si kikwazo kwani nyumba zinaendelea kujengwa kwa kasi.

Aidha uchunguzi huo umebaini pia kuwa asilimia kubwa ya wananchi waliojenga nyumba katika mazingira hayo waliyavamia wakijua kuwa ni sehemu salama ya makazi lakini sasa imekuwa ni majuto kwani nyumba zao zipo katika hatari ya kumezwa na makorongo hayo yanayoendelea kutanuka siku kwa siku.

Kama hiyo haitoshi Mecira ilikutana na jamii ya kabila la wamasai ambao wanachunga ng’ombe katika mlima huo wa Mindu,walipoulizwa kuwa kwa nini wanalisha mifugo yao kwenye hifadhi ya mlima huo walibainisha kuwa wapo katika eneo hilo kwa muda sasa na wameshayaozea maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live