Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa kuipokea treni ya mizigo Moshi

66817 Pic+pm

Mon, 15 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua treni ya mizigo Jumamosi ya Julai 20, 2019 Mkoani Kilimanjaro.

Treni hiyo itapokelewa Mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa na mabehewa 20 iliyobeba mifuko 20 ya saruji.

Kwa zaidi ya miaka 13 safari za treni hizo zilisimama kufanya kazi katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kutokana na sababu mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 15, 2019 amesema Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

Hata hivyo Mwananchi limepita katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kushuhudia usafi ukifanyika katika barabara za reliĀ  huku baadhi ya wananchi wakishangaa kuona kichwa cha treni kikipita maeneo mbalimbali.

Jana usiku kichwa cha treni kilipoonekana kikipita katika baadhi ya maeneo Mjini Moshi wananchi mkoani humo walianza kushangilia kwa furaha huku wengine wakipiga kelele za furaha.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz