Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa kuanza ziara ya siku nne Kigoma

Sat, 16 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuwasili mkoani Kigoma Februari 16, 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

Akizungumza leo Ijumaa Februari 15, 2019 mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga amesema Majaliwa atatembelea wilaya ya Kigoma, Uvinza, Kibondo na Kakonko.

Amesema lengo la ziara yake hiyo ni kuweka mkazo na msisitizo katika ufufuaji na uendelezaji wa zao la chikichi ikiwa na pamoja kukagua vitalu, mashamba, lengo likiwa ni uboreshaji wa zao hilo.

Amesema akiwa mkoani humo Waziri Mkuu atatembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo na kuzungumza na wakimbizi.

Amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine ataangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya CCM na kukagua miradi mbalimbali pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo atakayokuwa anakutana nao.

"Niwaombe wananchi na wakazi wa mkoani hapa, kujitokeza kwa wingi kumpokea Waziri Mkuu kama ilivyo desturi yetu mpaka atakapomaliza ziara yake na kuelekea mkoani Kagera,"amesema Maganga.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz