Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa azionya halmashauri zinazosuasua ukusanyaji mapato

67975 Pic+majaliwa

Tue, 23 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Waziri Mkuu wa Tanzania , Kassim Majaliwa ameziagiza halmashauri zinazosuasua katika ukusanyaji wa mapato kujitathmini.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 23,2019 katika mkutano mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) jijini Mwanza.

Majaliwa aliyemuwakilisha Rais John Magufuli amesema halmashauri zinazoshika mkia katika ukusanyaji huo ziangalie zilipojikwaa.

"Halmashauri za mwisho fanyeni tathimini wapi mmejikwaa, kwa nini mmeshindwa kufikia malengo, mfano Mkoa wa Kigoma halmashauri nyingi hazijafanya vizuri pamoja na Ruvuma,” amesema Majaliwa.

Amezitaka pia kusimamia makusanyo kupitia vyanzo vya mapato vya ndani ili kujiendesha mwaka 2020/25, kutaka fedha zinazokusanywa kuelekezwa katika shughuli za maendeleo.

Chanzo: mwananchi.co.tz