Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa awasili Kigoma kwa ziara ya siku nne

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo mchana Jumamosi Februari 16, 2019 amewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne.

Kiongozi huyo amepokewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa huo, akitarajiwa kutembelea katika Wilaya ya Kigoma, Uvinza, Kibondo na Kakonko.

Mbali na kutembelea Wilaya hizo, pia atazungumza na wananchi pamoja na wakimbizi katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo.

Katika ziara yake waziri Mkuu, pamoja na mambo yote ataangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya CCM na kukagua miradi mbalimbali pamoja na kuongea na wananchi katika maeneo atakayokuwa anakutana nao.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz