Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa awapa maagizo wakuu wa mikoa nane

62829 Majaliwapic

Sat, 15 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa nane nchini Tanzania kuhakikisha ndani ya mwaka mmoja kukamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumamosi Juni 15, 2019 katika ufunguzi wa kongamano la nne la uwezeshaji wananchi kiuchumi lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lenye kauli mbiu ‘Wezesha Watanzania Kujenga Viwanda.’

Taarifa iliyotolea na ofisi ya waziri mkuu, imenukuu Majaliwa akiitaja mikoa hiyo kuwa ni  Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Singida na Shinyanga.

Majaliwa amewataka viongozi wa mikoa na halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi,  kama cha Wilaya ya Kahama ili kuharakisha nia ya Serikali katika kuwezesha wananchi kiuchumi.

Kwa upande wa Mikoa iliyokamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji, imetakiwa kuonesha hatua za utekelezaji katika kutumia fursa mbalimbali zilizoainishwa pamoja na mikakati ya kutangaza fursa hizo zilizopo katika maeneo yao ifikapo 2019.

Pia, Majaliwa ametumia fursa hiyo kuiagiza NEEC, kuratibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo ya Serikali na ile ya binafsi ili kujua idadi yake na wanufaika kupelekewa taarifa.

Pia Soma

Amesema matokeo ya tafiti ziliyofanywa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuhusu biashara na uwekezaji nchini unatarajia kuchangia kwa kiasi kikubwa  uandaaji wa maandiko ya miradi mikubwa inayopendekezwa na shirika hilo.

“Miradi hiyo ni pamoja na ule wa “Harmonized Innovation Solutions for Local Economic Development” ambao upo katika hatua za maandalizi. Lengo la UNDP ni kuhakikisha kuwa miradi inayohusu uwezeshaji wananchi kiuchumi inatekelezwa moja kwa moja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambalo lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu,” amesema.

Amesema NEEC ina uwezo mkubwa katika kusimamia miradi mbalimbali ya uwezeshaji ambayo inafadhiliwa na Serikali pamoja na jumuiya ya Kimataifa ikiwemo UNDP, ILO, UNCTAD, AfDB na UN-Women.

Ameyahakikishia mashirika hayo kuwa Serikali itasimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi yote ili kupata matokeo yaliyo tarajiwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz