Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa atua Kigoma

66643 Waziripic

Sun, 14 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Waziri Mkuu wa Tanzania,  Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Amewasili mkoani humo leo Jumamosi Julai 13, 2019 saa 5 asubuhi.

Katika ziara hiyo Majaliwa atatembelea miradi ya maendeleo na kufuatilia utekelezaji  wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015.

Akiwa mkoani humo ataongoza kongamano la Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) la kumpongeza na kumuombea Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Baadaye atatembelea kituo cha utafiti wa zao la mchikichi Kihinga na kukutana na viongozi wa chama na Serikali.

 

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz