Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa atoa miezi miwili walilochangia upotevu zaidi ya Sh767milioni kuzirejesha

Majaliwa Pic Data Majaliwa atoa miezi miwili walilochangia upotevu zaidi ya Sh767milioni kuzirejesha

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa miezi miwili kwa watumishi wa Halmashauri ya Sengerema waliochangia upotevu wa zaidi ya Sh767 milioni kuhakikisha zinarudi.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Mei 7 katika ukumbi wa Sekondari ya Sengerema alipozungumza na watumishi wa halmashauri akiinukuu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inayobainisha Sh652 milioni zilipotea kwa kutopelekwa benki.

Ripoti hiyo pia imebaini Sh115 milioni zilipotea baada ya watumishi kuzima mashine ya kukusanyia mapato maarufu kama POS.

Hivyo, amemuagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, Frank Mkilanya kuchunguza kwa kina kubaini wahusika wa ubadhirifu huo na kuwachukulia hatua za kisheria.

Sambamba na agizo hilo Majaliwa amewataka watumishi kuwa waadilifu wanapotekeleza majukumu yao kwa kuacha kutafuna fedha za Serikali.

Vilevile, amewataka wakuu wa mikao na wilaya kusoma utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye vikao vya kamati ya siasa.

Advertisement Diwani wa Igalula, Sanije Shibiliti amesema Serikali kuanza kufuatilia upotevu wa fedha za umma kutaleta nidhamu kwa watumishi kuwa na nidhamu na matumizi yake.

Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu amesema wizi wa fedha za wananchi kwa watumishi wa halmashauri hiyo umekithiri hivyo kwa maagizo ya waziri mkuu watajiepusha kwa kufahamu kwamba watafuatiliwa.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz