Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa amtaka Mkandarasi VETA kufanya kazi usiku na mchana

Majaliwapic Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mkandarasi anayejenga chuo cha VETA Wilayani Chunya Mkoani Mbeya kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa chuo hicho kwa muda uliokusudiwa na Wana-Chunya waanze kupata mafunzo kuanzia mwezi Februari 2022,

Ametoa agizo hilo leo Novemba 29, 2021 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya.

Amesema kuwa malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kila makao makuu ya mikoa kunajengwa chuo kikubwa cha VETA

Chuo cha VETA cha Wilaya ya Chunya kitakachogharimu shilingi bilioni 1.6 kinajengwa katika kata ya Mbugani,kinatarajiwa kuhudumia jumla ya kata 20 zenye wakazi wasiopungua 211,039.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live