Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa ambana DED Tunduru gari la shule

66cc7eb4adbb30ba4e9f8a34136b5734 Majaliwa ambana DED Tunduru gari la shule

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempa siku mbili Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoni Ruvuma, Gaspar Balyomi awe amepeleka gari katika Shule ya Sekondari Tunduru kwa ajili ya kuwahudumia walimu na wanafunzi shuleni hapo.

Alitoa agizo hilo jana alipokagua ukarabati wa Shule ya Sekondari Tunduru. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya mbunge wa Tunduru Kusini, Daimu Mpakate kumueleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya usafiri.

“Mkurungezi Jumatatu lete gari moja hapa likiwa limeandikwa Shule ya Sekondari Tunduru, lije kutoa huduma kwa watoto na walimu wetu. Hii shule ina wanafunzi zaidi ya 600 na walimu 28 lazima iwe na usafiri ambao hata mtoto akiugua afikishwe hospitali,”alisema.

Kuhusu ukarabati uliofanyika shuleni hapo, Waziri Mkuu alisema alisema ameridhishwa na alimpomgeza Mkuu wa Shule, Amini Limia na kamati ya ujenzi kwa kazi nzuri ya usimamizi waliyoifanya.

Majaliwa alisema Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani, ilianzisha mkakati wa kukarabati shule zote kongwe nchini ikiwemo ya Shule ya Sekondari ya Tunduru, ambayo ukarabati wake umegharimu zaidi Sh milioni 700. Mkoa wa Ruvuma umepewa Sh bilioni 3.7 kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe za sekondari ikiwemo ya Tunduru.

Pia, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi wazingatie sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa shuleni hapo ili waweze kuishi vizuri.

“Someni hasa sasa hivi ni wakati wa likizo mpo hapa mnaendelea na masomo, hatutarajii mpate daraja la nne wala sifuri. Kila mmoja ahakikishe anasoma na kupata daraja litakalomfikisha chuo kikuu,” alisema.

Majaliwa alisema amefurahishwa na ufualu wa wanafunzi wa shule hiyo katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo, kwani wanafunzi wote wa kidato cha sita walifaulu kwa zaidi ya asilimia 90 na kuwa anatarajia katika matokeo ya mwaka huu watafaulu kwa asilimia 100.

Awali, Mkuu wa shule hiyo, Limia alisema walipokea zaidi ya Sh milioni 792 serikalini kupitia mpango wa EP4R kwa ajili ya ukarabati wa majengo 15, ambayo yalikuwa yanakabiliwa na uchakavu mkubwa kutokana na kujengwa miaka 38 iliyopita.

Alisema ukarabati huo pia ulihusisha ujenzi wa majengo mengine mawili, ambayo ni matundu 12 ya vyoo kipya cha wanafunzi na kibanda cha mlinzi.

“Majengo yaliyokarabatiwa ni jengo la utawala, bwalo, jiko, madarasa vyumba 16, mabweni sita, jengo la zahanati, jengo la duka, stoo, vyoo, majengo manne na mfumo wa maji taka nje ya majengo,” alisema.

Shule ya Sekondari Tunduru ni miongoni mwa shule kongwe nchini ambayo ilianzishwa mwaka 1982. Ni shule ya wavulana kwa kidato cha tano na sita katika michepuo ya PCM, PCB, PGM, CBG, HGL, HGK NA HKL na ina jumla ya wanafunzi 682 na walimu 28

Chanzo: habarileo.co.tz