Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa akabidhi nyumba, fedha milioni 18.9 kwa mlemavu Tanga

70ae63fd44fa815bf3b152fb3480515c.png Majaliwa akabidhi nyumba, fedha milioni 18.9 kwa mlemavu Tanga

Fri, 22 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemkabidhi nyumba yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 40 mkazi wa Korogwe mkoani Tanga, Miriam Shemndolwa ambaye ni mlemavu wa viungo.

Majaliwa amemkabidhi binti huyo hati ya nyumba hiyo aliyoagiza ajengewe ili iweze kumsaidia katika maisha.

Pia Miriam alichangiwa Sh milioni 18.9 kwa ajili ya kumuwezesha kuanzisha shughuli za kumuingizia kipato.

Katika fedha hiyo aliyochangiwa leo, Rais Dk John Magufuli alichangia Sh milioni 10, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alitoa Sh milioni tano, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa laki tano, na kiasi kilichobaki kilitolewa na viongozi wa serikali pamoja na wananchi.

Chanzo: habarileo.co.tz