Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa aeleza miaka mitano ya JPM Arusha

5ff636a96ae0ab181cda170be6f8c9d2 Majaliwa aeleza miaka mitano ya JPM Arusha

Mon, 14 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina mkataba na chama chochote cha siasa kushirikiana kwenye nafasi ya Rais, ubunge na udiwani.

Pinda alisema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge katika Jimbo la Vunjo kumnadi mgombea wa chama hicho, Dk Charles Kimei.

“Mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu, hakuna sehemu tumekubaliana na wala sijatumwa kuja kusema makubaliano yoyote, ninyi chagueni mafiga matatu, Rais, Mbunge na madiwani wa CCM, hao wengine tutaendelea kuwa marafiki lakini siyo katika kushika dola,” alisema Pinda.

Alisema CCM ina utaratibu wake kupata wagombea na haijafanya makubaliano na mgombea yeyote nje ya wale wa CCM na kwamba dhamana pekee wanayoahidi kwa wananchi ni kuwaletea maendeleo.

Aidha, Pinda alisema serikali ya awamu ya tano imefanya mapinduzi makubwa katika utekelezaji wa sekta za elimu, afya, miundombinu, umeme na uchumi.

Aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua Magufuli nafasi ya urais na Dk Kimei katika nafasi ya ubunge, kwa kuwa serikali imefanikiwa kukusanya kodi kutoka Sh bilioni 850 mwaka 2015 hadi zaidi ya Sh trilioni 1.3 kwa mwezi mwaka 2020 kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wananchi.

“Yapo mengi ya kusema, mfano mdogo tu, kodi kutokana na madini ilikuwa Sh bilioni 1.6 mwaka 2015, lakini hadi kipindi hiki tunaelekea katika uchaguzi mkuu kodi inayotokana na madini ni zaidi ya Sh bilioni 360.

Kodi hizi ndiyo zinaendesha miradi ya maendeleo, sasa mnataka nini?” alihoji Pinda.

Kwa upande wake, Dk Kimei aliwaomba wapiga kura wamchague kuwa Mbunge ili aweze kuanzisha mchakato wa kuunda halmashauri ya Vunjo kwa lengo la kurahisisha mawasiliano na huduma za kijamii na nyingine za kiutawala kutoka eneo la sasa la Kolila ambalo huongeza gharama kwa wananchi.

Alisema jimbo hilo lina changamoto nyingi ikiwamo miundombinu mibovu ya barabara, elimu, afya na ukosefu wa masoko ya mazao na kuaahidi akichaguliwa atazishughulikia.

Dk Kimei alisema atatumia uzoefu wake katika sekta ya fedha kuanzisha Mfuko wa Ujasiliamari wa Jimbo ili utoe mikopo nafuu kwa wanachi wa jimbo hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz