Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maiti za vichanga zapotea kiajabu hospitali ya mkoa

HOMERA Maiti za vichanga zapotea kiajabu hospitali ya mkoa

Thu, 25 Jun 2020 Chanzo: --

Homera alitoa agizo hilo jana, akisisistiza kuwa ni uzembe maiti kupotea ilhali wasimamizi wa chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo wapo.

Alisema watumishi katika chumba hicho wanapaswa kusimamishwa katika mara moja ili kupisha uchunguzi unaoendelea.

Kiongozi huyo wa mkoa alisema hakuna haja kuendelea kukaa na watumishi wanaosababisha shida katika idara, akihoji sababu za kupotea kwa maiti hizo na watumishi hao kutokujua zilikopelekwa ilhali wameajiriwa ili kuhakikisha hakujitokezi matatizo katika idara hiyo.

Hata hivyo, Homera alilihusisha tukio hilo na imani za kishirikina, akiwataka wanasiasa na wadau wa madini kutojihusisha na vitendo hivyo.

"Hatuwezi kusubiri mtu mwingine aje atatue matatizo ya Katavi wakati kuna mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya na viongozi wengine. Inaonekana kuna watu wanadanganywa, ukifanya hivyo utashinda uchaguzi, au utapata madini mengi, na huu mchezo unaonekana ulikuwapo," alisema.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa huo, Dk. Justina Tizeba, alidai kuwa siku ya tukio, alipokea taarifa kutoka kwa muuguzi mfawidhi zikimtaka afike hospitalini huko kwa kuwa kulikuwa na tatizo la kupotea kwa maiti mbili za watoto wachanga.

Alisema kuwa baada ya kufika hospitalini, waliwahoji watendaji katika chumba cha kuhifadhi maiti ambao walikiri kupokea maiti hizo na kuzihifadhi, lakini zilizotakiwa kutoka, hazikuonekana na hawakujua zilikokwenda.

Dk. Tizeba alisema kuwa walitoa taarifa kituo cha polisi na wahusika walikamatwa na kuwekwa mahabusi, lakini baadaye waliachiwa kwa dhamana.

Rebecca Faustine, mmoja wa wazazi wa walipoteza watoto hao muda mfupi baada ya kujifungua, alisema aliumwa uchungu Jumamosi na alipojifungua, hakujua alikopelekwa mtoto wake.

"Baadaye wifi yangu na mume wangu ilibidi wamuulize nesi 'mtoto yuko wapi?' Na nesi alijibu kuwa mtoto alifariki dunia, lakini walipoomba maiti wakazike, maiti haikuonekana hadi sasa," alisema.

Chanzo: --