Tarime. Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria jana Novemba 26, 2018 itazikwa katika eneo ilipotokea ajali hiyo kijiji cha Komaswa wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Akizungumza leo Jumanne Novemba 27, 2918 mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema uamuzi huo umechukuliwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kutokana na ushauri uliotolewa na kamati ya Taifa ya maafa.
Amesema hadi sasa majina 12 kati ya 16 ya waliofariki dunia yamejulikana licha ya miili yao kutotambulika kutokana na jinsi ilivyoungua.
“Isipokuwa miili miwili ambayo ilitambuliwa ukiwemo wa dereva na mwingine uliotambulika baada ya kukutwa na cheni shingoni,” amesema Malima.
Amesema mazishi hayo yatafanyika kesho Novemba 27, 2019 saa nne asubuhi, kwamba mabaki yaliyotokana na miili kuungua yatakusanywa na kuzikwa eneo hilo.
Amesema baada ya mazishi eneo hilo utajengwa mnara kwa ajili ya kumbukumbu.