Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahenge Ataka waajiri kuboresha mazingira ya kazi

9f77b11396254655488d772762083d36.jpeg Mahenge Ataka waajiri kuboresha mazingira ya kazi

Sun, 2 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewataka waajiri wote katika sekta za umma na binafsi kuboresha mazingira ya kazi ya wafanyakazi wao.

Aliwataka kushirikiana na vyama vya wafanyakazi katika ofisi zao na kutowabugudhi wanachama wao

Alitoa mwito jana katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma wakati wa Sherehe ya Wafanyakazi.

Mahenge aliwapongeza wafanyakazi wote kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii hali iliyosaidia nchi kuingia uchumi wa kati na kuwaomba waendelee kufanya kazi kwa bidi zaidi.

Mwenyekiti Tucta Mkoa wa Dodoma, Lizzy Msechu alimuomba mkuu huyo wa mkoa kuwasaidia kufikisha kilio cha wastaafu kucheweleweshewa mafao yao katika ngazi za juu ili kuwapa hamasa wafanyakazi waliopo kazini.

Chanzo: www.habarileo.co.tz