Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yatoa hati ya kuwakamata waliovujisha mitihani la saba

Mahakamaaaaaaa Mahakama yatoa hati ya kuwakamata waliovujisha mitihani la saba

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoka hati ya kuwatafuta na kuwakamata washtakiwa wawili wanaodaiwa kusambaza mitihani ya Taifa ya darasa la saba kwa njia ya mtandao wa kijamii Telegram baada ya kukiuka masharti ya dhamana.

Washtakiwa hao ni Jacob Adagi ambaye ni mshtakiwa wa 11 na Joel Ngome, mshtakiwa wa 12 katika kesi hiyo ya jinai.

Washtakiwa hao na wenzao 10, wakiwemo walimu wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya kuvujisha mitihani na kutengeneza nyaraka za uongo.

Uamuzi huo umetolewa Jana, Machi Mosi, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mazengo ametoa uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Faraji Ngukah kueleza kuwa washtakiwa hao hawajafika mahakamani tangu walipopata dhamana na hawana taarifa yoyote.

Hakimu Mazengo amesema ametoa hati ya kuwakamata washtakiwa hao, baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha maombi wakiomba mahakama hiyo itoe hati ya kuwakamatwa washtakiwa hao.

Mahakama imeshatoa hati nne za kuwakamata washtakiwa wawili baada ya kushindwa kufika mahakamani, washtakiwa hao ni, Lloyd Mpande na Ronald Odogo.

Awali, wakili Ngukah alidai kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo Hakimu Mazengo aliutaka upande wa mashtaka kukamilisha haraka upelelezi wa kesi hiyo.

" Hivi upande wa mashtaka mnaendelea kupeleleza nini? Watu wanatuhumiwa kuiba mitihani bado wanaendelea kufanya uchunguza hadi lini? Kamilisheni upelelezi" alielekeza Hakimu Mazengo.

Baada ya kutoa kauli hiyo, Hakimu ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 29, 2023 itakapotajwa.

Washtakiwa wengine ni Jahnson Ondieka (37), Patrick Chawawa, Theresia Chitanda, Elinami Sarakikya, Joyce Nyanyakila na Gladius Roman.

Wengine ni Dorcas Muro na Alcheraus Malinzi.

Katika mashtaka yao, mshtakiwa Malinzi anadaiwa kati ya Oktoba 2, 2022 na Oktoba 12, 2022 sehemu isiyojulikana mshtakiwa huyo akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo wa  mtihani wa somo la uraia la  darasa la saba akijifanya mtihani huo ni halali na umeandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta)

Pia, tarehe hiyo na sehemu isiyojulikana mshtakiwa Malinzi akiwa na nia ya kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo wa mitihani wa somo la Maarifa ya Jamii wa darasa la saba uliojifanya mwaka 2022, alionyesha kuwa mtihani huo umeandaliwa na Necta.

Katika shtaka tatu, mshtakiwa Adagi na Ngome wanakabiliwa na shtaka moja la kuvujisha mitihani ya Taifa ya darasa la saba, kinyume cha sheria.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Oktoba 19, 2022. Hata hivyo washtakiwa hao wapo nje kwa dhamana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live