Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaamuru nyumba kubomolewa kisa deni la Milioni 3

Dsc1687 0 O Mahakama yaamuru nyumba kubomolewa kisa deni la Milioni 3

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imeamuru kubomolewa kwa nyumba ya Rajabu Mukoko, maarufu Osama, na mali zake kupigwa mnada kufidia Sh. milioni tatu, baada ya kushindwa katika shauri la kujimilikisha na kuuza ardhi ya Hidaya Seleman Issa (68), kinyume cha sheria.

Mukoko aliuziwa eneo hilo na aliyekuwa mume wa Hidaya, Twalib Amri, waliyetengana naye mwaka 2015 kisha mama huyo kuanza kupigwa na kuzuiwa kufika katika eneo hilo na aliyekuwa mume wake.

Mgogoro huo umedumu kwa miaka minane tangu mwezi Juni, 2016 huku mdaiwa namba moja akiwa Twalib Amri (mume wa zamani wa Hidaya) na Rajabu Mukoko (aliyeuziwa eneo hilo) kushindwa kesi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live