Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaamuru mwili wa marehemu ufukuliwe

Mahakama Mpandaaaa Mahakama yaamuru mwili wa marehemu ufukuliwe

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, imeamuru mwili wa marehemu, Juma Andrea Bukuku uliyokuwa umezikwa ufukuliwe na kuzikwa upya, baada ya mjane wake, Rehema Said kushinda shauri alilofungua kwamba mumewe amezikwa kinyume na imani ya dini yake.

Mjane huyo aliomba mahakama itoe amri ya kufukuliwa mwili huo na kuzikwa upya kwa imani ya dini ya Kiislamu, badala ya dini ya Kikristo iliyotumika wakati wa mazishi ya awali yaliyofanyika Aprili 17, 2024 katika makaburi ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda. Juma Andrea Bukuku alifariki Aprili 15, mwaka huu.

Akitoa uamuzi wa shauri hilo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Gasper Luoga, amesema amepitia ushahidi uliotolewa na upande wa mdai ukiongozwa na Rehema Said aliyekuwa mke wa marehemu, pamoja na ushahidi wa mdaiwa ukiongozwa na Andrea Bukuku, ambaye ni baba wa marehemu na kuridhika na ushahidi wa mdai.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live