Mahakama ya Wilaya ya Arusha Mkoani Arusha imetoa amri kwa Wajibu maombi watatu ambao ni Innocent Mwanga, Robert Owenya pamoja na Josephat Temu na wenzake kuzuiwa kuendesha mazishi ya Mfanyabiashara wa madini Marehemu Christian Temu na kuamuru Mke wa Marehemu Yasita Kilawe ndiye ahusike kuendesha na kusimamia mazishi ya Mume wake.
Mahakama hiyo imesema ni muhimu Mke huyo wa Marehemu kushirikishwa kwa kuwa ana haki na kwamba ni wazi kitendo kilichofanywa na Wajibu maombi hao cha kumuengua kwenye mipango ya mazishi na kuchagua sehemu ya kumzika bila kumshirikisha kimemnyima haki Mke huyo wa Marehemu.
Yasinta aliwasilisha maombi hayo Mahakamani na kutaka Ndugu wa Marehemu Mume wake wazuiwe kuzika kwa kuwa hakushirikishwa awali kwenye taratibu za mazishi hali iliyopelekea sitofahamu katika msiba huo.
Ikumbukwe kuwa jana October 1 ndiyo ilikua imepangwa mazishi hayo yafanyike ambapo licha ya maandalizi yote kukamilika ikiwemo kaburi kuchimbwa, Ndugu hao walishindwa kuuzika mwili wa Christian Temu baada ya Mke wa Marehemu Yasinta Kilawe kuweka zuio Mahakamani.