Morogoro. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu nchini Tanzania, Jenista Mhagama amesema wizara hiyo imewasaidia vijana 18,800 wa halmashauri za wilaya 88 kupata mafunzo ya teknolojia ya kitalu nyumba ili waweze kujiajiri.
Mhagama ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 mkoani Morogoro katika ufunguzi wa maonyesho ya 29 ya Nanenane Kanda ya Mashariki.
Amesema jambo hilo linawezekana kufanyika nchi nzima, kuna uhakika wa kuwa moja ya fursa za ajira kwa vijana wengi.
Amebainisha kuwa wataendelea kutoa mafunzo katika sekta ya ufugaji wa samaki kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
‘’Sekta za kilimo, mifugo na uvuvi vinaweza kuwa ajira mbadala kwa maisha ya kijana wetu wa Kitanzania hivyo lazima tuwawezeshe katika kila hali na hatua mbalimbali,” alisema waziri huyo.
Kuhusu wakulima, Mhagama amesema wataendelea kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo kama matrekta, mashine za kupandia na kuvunia mpunga pamoja na za kupukuchua mahindi.
Pia Soma
- Wahofia kuondolewa kwenye maeneo ya kufanyia biashara
- Rais John Magufuli kuzindua Terminal 3 muda mfupi ujao
- Uhamiaji Tanzania yachukua paspoti saba nyumbani kwa Kabendera
- Serikali ya Tanzania yasaini mkataba ujenzi barabara ya lami Tanga - Pangani