Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magugu maji yasimamisha vivuko katikati ya safari Mwanza

89854 Magugu+pic Magugu maji yasimamisha vivuko katikati ya safari Mwanza

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Usafiri wa kivuko kati ya Kigongo Wilaya ya Misungwi na Busisi Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza nchini Tanzania umesimama kwa zaidi ya saa moja kutokana na magugu maji kutanda katika njia inayotumiwa na vivuko.

Leo Jumanne Desemba 24, 2019 vivuko viwili vya Mv Mwanza na Mv Misungwi vinavyosafirisha abiria, mizigo na magari katika eneo hilo vimelazimika kusimama katikati ya maji vikishindwa kwenda wala kurudi nyuma.

Mmmoja wa abiria katika kivuko cha Mv Mwanza aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina amesema jitihada ya zaidi ya saa nzima ya kuyasukuma magugu maji hayo hazijazaa matunda na hivyo vyombo hivyo kulazimika kusimama katikati ya maji kusubiri yasukumwe kwa upepo.

“Tuko hapa tangu saa 11:00 jioni hadi sasa saa 12:25 bado tuko hapa hatujui tutatoka saa ngapi,” amesema abiria huyo

Akizungumza na Mwananchi kwa simu, Mkuu wa Kivuko cha Kigongo-Busisi, Abdallah Atiki amesema juhudi za kusukuma magugu maji hayo kutoka kwenye njia zilifanyika.

“Kwa usalama wa abiria na vyombo vyetu, vivuko haviwezi kutembea wakati kuna magugu maji; inapotokea hali kama hii huwa tunatumia vyombo vyetu vingine kuyasukuma magugu maji kabla ya kurejesha huduma,” amesema Atiki

Kwa siku, vivuko vya Mv Mwanza na Mv Misungwi husafirisha kati ya abiria 6,500 hadi 8,000 na magari zaidi ya 730.

Tayari Serikali imetangaza kuanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilomita 3.2 kuunganisha eneo la Kigongo- Busisi kuondoa adha ya usafirishaji katika eneo hilo.

Mradi wa ujenzi wa daraja lenye njia nne kwa gharama ya zaidi ya Sh699 bilioni utakamilika mwaka 2024.

Chanzo: mwananchi.co.tz