Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli azindua barabara akishangaa wingi wa matuta

78730 Barabara+pic

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameshangazwa na idadi kubwa ya matuta katika barabara ya Tunduma- Sumbawanga na kueleza kuwa inaweza kuwa barabara inayoongoza duniani kwa matuta.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 6, 2019 wakati akizindua barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 223.1.

“Barabara nzuri ila imezidi matuta jamani, sijawahi kuona barabara yenye matuta kama hii inaweza kuongoza duniani. Hii inaweza kuwa na maana kwamba madereva hawatumii vizuri barabara.”

“Sasa kila yanapokuwa yanachoka myatoe, muweke alama watanzania wanajitambua ila utasikia wengine wanasema watu watagongwa mara mbuzi wanagongwa sasa uliwaleta wa nini barabarani,” amesema Magufuli.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwakumbusha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutoruhusu barabara hiyo kuwa chanzo cha ajali katika Mkoa wa Rukwa.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz