Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli awabana MA-DC, awataka wakabiliane na wavivu

Ee432d2035f254e6cbab82ecc06650c6 Magufuli awabana MA-DC, awataka wakabiliane na wavivu

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS John Magufuli amewataka wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha wananchi wanafanya kazi kwani hatotoa chakula kwa mkoa wowote utakaokumbwa na njaa.

Magufuli ameyasema hayo akiwa wilaya ya Bahi wakati akirejea jijini Dodoma leo huku akieleza kushangazwa na wananchi wa wilaya hiyo ambao hawatumii fursa ya mvua na mito inayotiririsha maji kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Awali Mbunge wa Bahi, Kenneth Nallo alimwambia Rais Magufuli kuwa moja ya changamoto iliyopo jimboni kwake ni wananchi kutopenda kufanya kazi.

“Mheshimiwa Rais, nashukuru nimepata DC mzuri na Mkurugenzi mzuri...ni wachapa kazi, tumeshirikiana kuhakikisha tunapambana na wananchi wetu ili wafanye kazi, wengi ni wavivu hawapendi kufanya kazi,” alisema.

Akizungumzia hilo, Rais Magufuli alisema: “Watani zangu Wagogo, fanyeni kazi, nawaomba sana, limeni, mvua inanyesha limeni mpunga, limeni viazi, uwele, ukienda Morogoro wakina mama wamepanga viazi barabarani wanauza, havikushushwa kutoka mbinguni vile, wamelima wamefanya kazi.

“Huko nilikotoka mpaka Kahama, Tabora watu wanalima, nimefika kuanzia Manyoni sioni anayelima, mvua hamuioni? maji yanatiririka kwenye mito hamuoni?" alihoji.

“Nikiwangalia hapa nawaona wote mna afya njema, nilitegemea kijana wa miaka 18 aniombe shamba lakini hamna,

“Niwambie wazi, sitatoa chakula kwenye Wilaya yoyote, hakuna chakula cha bure kama mlivyozoea huko nyuma, usipofanya kazi usile na usipokula kufa, lazima tuambiane ukweli, watu wafanye kazi, walime, na asiyefanya kazi asile.

"Na Mkuu wa Wilaya ambaye Wilaya yake itapata njaa DC ataondoka na Viongozi wengine wanaostahili kuhamasisha wananchi kufanya kazi wataondoka, tunataka pesa tunayopata ifanye kazi nyingine, tunatoa elimu bure, tunajenga SGR ndio kazi za Serikali, sio kukulisha, haiwezekani mwingine alime shamba mahindi yanatoa mbelewele mwingine halimi chochote, kwangu bure hamna, mfanye kazi.” alisema Magufuli.

Chanzo: habarileo.co.tz