Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli atengua uteuzi wa DED

65132 Pic+tamisemi

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Lucy Mganga kutokana na utendaji kazi wake usioridhisha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 1, 2019 jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo amesema uteuzi wa kujaza nafasi hiyo itajazwa hapo baadaye.

Pia, Jafo amewataka wakuu wa mikoa (RC) wenye jukumu la ujenzi wa Hospitali za Wilaya katika maeneo yao kuzingatia muda wa kukamilisha ujenzi uliotolewa ambao ulikuwa Juni 30, 2019 pamoja na kuhakikisha taarifa ya ujenzi sambamba na picha imeshawasilishwa Ofisi ya Rais Tamisemi kwa hatua zaidi.

Chanzo: mwananchi.co.tz