Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli agiza wananchi kutochangishwa Sh25,000 mkoani Songwe

78436 Pic+magu+michango

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Songwe.Rais wa Tanzania, John Magufuli amemuagiza mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali mstaafu Nicodemus Mwangela kufanya uchunguzi wa fedha wanazochanga wananchi kwa ajili ya shule za msingi kata ya Myovizi wilayani Mbozi.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 baada ya wananchi wa eneo la Mahenge kulalamikia wingi wa michango ukiwamo wa Sh25,000, kuagiza kiasi hicho cha fedha kutochangishwa tena.

Magufuli yupo katika ziara ya siku tatu mkoani Songwe kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, amekuwa akizungumza na wananchi katika maeneo anayopita.

 “Mkuu wa mkoa uje kufuatilia fedha zote zilizochangwa kwa wananchi, hawawezi kuchangishwa fedha zote hizi, ningekuwa mbunge nisingeruhusu wananchi wachangishwe,” amesema Rais Magufuli aliyewachangia wananchi hao Sh5 milioni na kufuta mchango wa Sh25,000.

Awali,  mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga  amesema michango inayochangishwa kwenye jimbo hilo inaasisiwa na ofisi ya wilaya.

Amesema amekuwa akisoma mapato na matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo ambazo hupelekwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa madarasa na zahanati.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz