Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli aagiza bibi wa miaka 94 kurejeshewa ardhi

79465 Ardhi+pic

Fri, 11 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro. Rais John Magufuli ameagiza Martha Kuzilwa (94) mkazi wa kijiji cha Losinyai wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kurudishwa ekari 300 alizoporwa.

Akizungumza na Martha jana Jumatano Oktoba 9, 2019 baada ya kumtembelea nyumbani kwake, Mnyeti amesema Rais Magufuli amemuagiza kusimamia suala hilo ili bibi huyo arejeshewe ardhi.

Amesema baada ya kuwepo mgogoro wa muda mrefu baina ya bibi huyo na waliovamia eneo lake, aliwasilisha kilio chake kwa Magufuli aliyeagiza arudishiwe shamba lake.

"Baada ya kufika kwa bibi huyu na kuwasikiliza viongozi wa vijiji na majirani wametuhakikishia shamba ni lake, anapaswa kurudishiwa kwani wajanja wachache walimpora," amesema.

Amesema ameacha maagizo kwa mkuu wa wilaya ya Simanjiro,  Zephania Chaula ili Jumamosi Oktoba 12, 2019 akabidhiwe  shamba lake.

Chanzo: mwananchi.co.tz