Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli aagiza Sh100 milioni kuongezwa mradi wa maji Vwawa

78466 Pic+magu+ardhi

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika mji wa Vwawa mkoani Songwe na kumuagiza  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuongezea Sh100 milioni katika mradi huo.

Akizungumza katika ziara ya siku tatu ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo aliyoanza leo Ijumaa Oktoba 14, 2019 mkoani humo,  Magufuli amesema amesema anachotaka kuona ni uhakika wa maji kwa wananchi wa Songwe.

“Nataka kuona maji yakimwagiza kwenye eneo hili ili wananchi wapate kwa uhakika,” alisema Rais Magufuli.

Pia, kiongozi huyo wa nchi amezindua kiwanda cha kukoboa kahawa cha GDM chenye uwezo wa kukoboa tani 8.3 kwa saa moja.

“Kiwanda hiki ni wazalendo kwa hiyo wakihitaji mkopo wapewe na hakikisheni wafanyakazi wanapata mishahara ya uhakika, wasaidieni vijana hawa,” amesema Rais Magufuli.

Chanzo: mwananchi.co.tz