Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magoti aapishwa kuwa DC Kisarawe

Magoti Aapishwa Kuwa DC Kisarawe Magoti aapishwa kuwa DC Kisarawe

Fri, 14 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge leo June 14,2024 amemuapisha Petro Magoti Itozya (aliyekuwa Msaidizi wa Rais upande wa siasa), kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Uapisho umefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani iliyopo Kibaha na kuhudhuriwa na Wakuu wa Wilaya wengine wa Wilaya za Pwani, Viongozi wa Dini na Serikali na Wageni wengine waalikwa.

Itakumbukwa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alimteua Petro Magoti kuwa DC wa Kisarawe June 06,2024 akichukua nafasi ya Fatma Almas Nyangasa ambaye amehamishiwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live