Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Jafari Magesa (31) mkazi wa Milambo kwa tuhuma za kuunda njama za kumuua mtalaka wake aitwaye Gaudensia Shukuru (25) mkazi wa Malunga Manispaa ya Kahama.
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, SACP Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea May 27 mwaka huu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Wendele za uwepo wa mwili wa mwanamke aliyeuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali.
SACP Magomi amesema kuwa upelelezi wa awali wa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa talaka kati ya marehemu na aliyekuwa mumewe, ambapo walikuwa na kesi mahakamani juu ya talaka ambayo ilikuwa itolewe hukumu yake May 28, 2024.