Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magari zaidi ya 100 yakwama barabara ya Dar- Iringa Tanzania

Magari zaidi ya 100 yakwama barabara ya Dar- Iringa Tanzania

Tue, 4 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Magari zaidi ya 100 yamekwama katika eneo la Mpunguzi jijini Dodoma nchini Tanzania kwa zaidi ya saa nane baada ya magari matatu ya mizigo kunasa kwenye tope kutokana miundombinu mibovu ya barabara iliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza  na Mwananchi leo Jumanne Februari 4, 2020 mmoja wa wasafiri, Victor Msigwa amesema magari  yaliyokwama ni kutoka Mkoa wa Iringa kwenda mikoa mingine kupitia Dodoma mjini na kutoka Dodoma kwenda mkoani Iringa.

Hata hivyo, amesema mvua zinazoendelea kunyesha zimeharibu miundombinu katika eneo hilo hivyo kusababisha magari matatu ya mizigo kutoka mkoani Iringa kukwama katika eneo hilo hivyo kusababisha magari mengine kushindwa kupita.

"Magari yameshindwa kupita baada ya magari matatu ya mizigo kunasa kuanzia saa sita usiku, hali hii inasababisha magari zaidi ya 100 kushindwa kupita, unachokifanya ni kujaribu kuyanasua magari hayo ili kuweza kupita," amesema Msigwa.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz